Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, jeshi la utawala wa Kizayuni lilianza tena mashambulizi dhidi ya Gaza kufuatia madai yaliyotolewa kuhusu shambulio dhidi ya gari la kivita la utawala huo huko Rafah.
Kufuatia madai ya mlipuko wa gari hilo la kivita na kutangazwa kwa vifo vya wanajeshi wawili wa Kizayuni na kujeruhiwa kwa wengine wawili, chaneli ya 14 ya utawala wa Kizayuni ilitangaza kwamba jeshi la anga lilishambulia maeneo yaliyolengwa katika eneo la Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Chaneli ya 12 ya Israel pia ilitangaza kwamba Netanyahu alikuwa akitathmini hali ya kiusalama huko Gaza na waziri wa vita na maafisa wa jeshi.
Wakati huo huo, chaneli ya 12 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni, ikinukuu vyanzo vyenye ujuzi, imeeleza mashambulizi haya kuwa ni jaribio la Wazayuni la kuwalinda wanamgambo wanaohusishwa na Yasser Abu Shababu.
Your Comment